Native Bible

Ruth 2:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Boazi akamuuliza msimamizi wa wavunaji, “Je, yule mwanamwali ni wa nani?”

Ruth 2:5 in English

Ruth 2:5 · Berean Standard Bible

And Boaz asked the foreman of his harvesters, “Whose young woman is this?”

Context

3Basi akaenda, akaokota mabaki ya nafaka mashambani nyuma ya wavunaji. Ikatokea kwamba alijikuta anafanya kazi kwenye shamba lililokuwa mali ya Boazi, ambaye alitoka kwenye ukoo wa Elimeleki. 4Papo hapo Boazi akarudi kutoka Bethlehemu, akawasalimu wavunaji, akasema, “Bwana awe nanyi!” Nao wakamjibu, “Bwana akubariki.” 5Boazi akamuuliza msimamizi wa wavunaji, “Je, yule mwanamwali ni wa nani?” 6Msimamizi akamjibu, “Ni yule Mmoabu aliyerudi kutoka nchi ya Moabu pamoja na Naomi. 7Yeye aliomba, ‘Tafadhali niruhusu niokote na kukusanya miongoni mwa miganda nyuma ya wavunaji.’ Naye ameshinda shambani tangu asubuhi pasipo kupumzika, isipokuwa kwa muda mfupi kivulini.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.