Warumi 9:15
Romans 9:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa maana Mungu alimwambia Mose, “Nitamrehemu yeye nimrehemuye, na pia nitamhurumia yeye nimhurumiaye.”
Romans 9:15 in English
Romans 9:15 · Berean Standard Bible
For He says to Moses: “I will have mercy on whom I have mercy, and I will have compassion on whom I have compassion.”*
Context
13Kama vile ilivyoandikwa, “Nimempenda Yakobo, lakini nimemchukia Esau.” 14Tuseme nini basi? Je, Mungu ni dhalimu? La, hasha! 15Kwa maana Mungu alimwambia Mose,
“Nitamrehemu yeye nimrehemuye,
na pia nitamhurumia yeye nimhurumiaye.” 16Kwa hiyo haitegemei kutaka kwa mwanadamu au jitihada, bali hutegemea huruma ya Mungu. 17Kwa maana Maandiko yamwambia Farao, “Nilikuinua kwa kusudi hili hasa, ili nipate kuonyesha uweza wangu juu yako, na ili Jina langu lipate kutangazwa duniani yote.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.