Native Bible

Romans 7:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Sitendi lile jema nitakalo kutenda, bali lile baya nisilolitaka, ndilo nitendalo.

Romans 7:19 in English

Romans 7:19 · Berean Standard Bible

For I do not do the good I want to do. Instead, I keep on doing the evil I do not want to do.

Context

17Lakini, kwa kweli si mimi tena nitendaye lile nisilotaka bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. 18Kwa maana ninafahamu kwamba hakuna jema lolote likaalo ndani yangu, yaani, katika asili yangu ya dhambi. Kwa kuwa nina shauku ya kutenda lililo jema, lakini siwezi kulitenda. 19Sitendi lile jema nitakalo kutenda, bali lile baya nisilolitaka, ndilo nitendalo. 20Basi kama ninatenda lile nisilotaka kutenda, si mimi tena nifanyaye hivyo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. 21Hivyo naiona sheria ikitenda kazi. Ninapotaka kutenda jema, jambo baya liko papo hapo.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.