Native Bible

Romans 5:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

nayo saburi huleta uthabiti wa moyo, na uthabiti wa moyo huleta tumaini,

Romans 5:4 in English

Romans 5:4 · Berean Standard Bible

perseverance, character; and character, hope.

Context

2ambaye kwa kupitia kwake tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo ndani yake sasa tunasimama, nasi twafurahia katika tumaini letu la kushiriki utukufu wa Mungu. 3Si hivyo tu, bali twafurahi pia katika mateso, kwa sababu tunajua kuwa mateso huleta saburi, 4nayo saburi huleta uthabiti wa moyo, na uthabiti wa moyo huleta tumaini, 5wala tumaini halitukatishi tamaa, kwa sababu Mungu amekwisha kumimina pendo lake mioyoni mwetu kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye ametupatia. 6Kwa maana hata tulipokuwa dhaifu, wakati ulipowadia, Kristo alikufa kwa ajili yetu sisi wenye dhambi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.