Native Bible

Romans 3:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kuna faida kubwa kwa kila namna! Kwanza kabisa, Wayahudi wamekabidhiwa lile Neno halisi la Mungu.

Romans 3:2 in English

Romans 3:2 · Berean Standard Bible

Much in every way. First of all, they have been entrusted with the very words * of God.

Context

1Basi kuna faida gani kuwa Myahudi? Au kuna thamani gani katika tohara? 2Kuna faida kubwa kwa kila namna! Kwanza kabisa, Wayahudi wamekabidhiwa lile Neno halisi la Mungu. 3Ingekuwaje kama wengine hawakuwa na imani? Je, kutokuamini kwao kungebatilisha uaminifu wa Mungu? 4La hasha! Mungu na aonekane mwenye haki, na kila mwanadamu kuwa mwongo, kama ilivyoandikwa: “Ili uthibitike kuwa wa kweli unaponena, na ukashinde utoapo hukumu.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.