Warumi 15:9
Romans 15:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
pia ili watu wa Mataifa wamtukuze Mungu kwa rehema zake. Kama ilivyoandikwa: “Kwa hiyo nitakutukuza katikati ya watu wa Mataifa; nitaliimbia sifa jina lako.”
Romans 15:9 in English
Romans 15:9 · Berean Standard Bible
so that the Gentiles may glorify God for His mercy. As it is written: “Therefore I will praise You among the Gentiles; I will sing hymns to Your name.”*
Context
7Karibishaneni ninyi kwa ninyi kama Kristo alivyowakaribisha ninyi ili kumletea Mungu utukufu. 8Kwa maana nawaambia kwamba, Kristo amekuwa mtumishi kwa wale waliotahiriwa ili kuonyesha kweli ya Mungu na kuthibitisha zile ahadi walizopewa baba zetu wa zamani, 9pia ili watu wa Mataifa wamtukuze Mungu kwa rehema zake. Kama ilivyoandikwa:
“Kwa hiyo nitakutukuza katikati ya watu wa Mataifa;
nitaliimbia sifa jina lako.” 10Tena yasema,
“Enyi watu wa Mataifa, furahini
pamoja na watu wa Mungu.” 11Tena,
“Msifuni Bwana, ninyi watu wa Mataifa wote,
na kumwimbia sifa, enyi watu wote.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.