Warumi 14:16
Romans 14:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Usiruhusu kile ambacho unakiona kuwa chema kisemwe kuwa ni kiovu.
Romans 14:16 in English
Romans 14:16 · Berean Standard Bible
Do not allow what you consider good, then, to be spoken of as evil.
Context
14Ninajua tena nimehakikishiwa sana katika Bwana Yesu kwamba hakuna kitu chochote ambacho ni najisi kwa asili yake. Lakini kama mtu anakiona kitu kuwa ni najisi, basi kwake huyo kitu hicho ni najisi. 15Kama ndugu yako anahuzunishwa kwa sababu ya kile unachokula, basi huenendi tena katika upendo. Usiruhusu kile unachokula kiwe sababu ya kumwangamiza ndugu yako ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake. 16Usiruhusu kile ambacho unakiona kuwa chema kisemwe kuwa ni kiovu. 17Kwa maana Ufalme wa Mungu si kula na kunywa, bali ni haki, amani na furaha katika Roho Mtakatifu. 18Kwa sababu mtu yeyote anayemtumikia Kristo kwa jinsi hii, anampendeza Mungu na kukubaliwa na wanadamu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.