Native Bible

Romans 11:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hii ni kweli. Matawi hayo yalikatwa kwa sababu ya kutokuamini kwake, lakini wewe umesimama tu kwa sababu ya imani. Kwa hiyo usijivune, bali simama kwa kuogopa.

Romans 11:20 in English

Romans 11:20 · Berean Standard Bible

That is correct: They were broken off because of unbelief, but you stand by faith. Do not be arrogant, but be afraid.

Context

18basi usijivune juu ya hayo matawi. Kama ukijivuna, kumbuka jambo hili: si wewe unayelishikilia shina, bali ni shina linalokushikilia wewe. 19Basi utasema, “Matawi yale yalikatwa ili nipate kupandikizwa katika hilo shina.” 20Hii ni kweli. Matawi hayo yalikatwa kwa sababu ya kutokuamini kwake, lakini wewe umesimama tu kwa sababu ya imani. Kwa hiyo usijivune, bali simama kwa kuogopa. 21Kwa maana kama Mungu hakuyahurumia matawi ya asili, wala hatakuhurumia wewe. 22Angalia basi wema na ukali wa Mungu: Kwa wale walioanguka, ukali, bali kwako wewe wema wa Mungu, kama utadumu katika wema wake. La sivyo, nawe utakatiliwa mbali.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.