Ufunuo 7:3
Revelation 7:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Msiidhuru nchi wala bahari, wala miti, hadi tuwe tumetia muhuri kwenye vipaji vya nyuso za watumishi wa Mungu wetu.”
Revelation 7:3 in English
Revelation 7:3 · Berean Standard Bible
“Do not harm the land or sea or trees until we have sealed the foreheads of the servants of our God.”
Context
1Baada ya hili nikaona malaika wanne wakiwa wamesimama katika pembe nne za dunia, wakizuia hizo pepo nne za dunia, ili kwamba pasiwe na upepo utakaovuma juu ya nchi au juu ya bahari au juu ya mti wowote. 2Nikaona malaika mwingine akipanda kutoka mawio ya jua akiwa na muhuri wa Mungu aliye hai. Akawaita kwa sauti kubwa wale malaika wanne waliokuwa wamepewa mamlaka ya kuidhuru nchi na bahari, akisema, 3“Msiidhuru nchi wala bahari, wala miti, hadi tuwe tumetia muhuri kwenye vipaji vya nyuso za watumishi wa Mungu wetu.” 4Ndipo nikasikia idadi ya wale waliotiwa muhuri: yaani 144,000 kutoka makabila yote ya Israeli. 5Kutoka kabila la Yuda 12,000 walitiwa muhuri,
kutoka kabila la Reubeni 12,000,
kutoka kabila la Gadi 12,000,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.