Ufunuo 3:11
Revelation 3:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Ninakuja upesi. Shika sana ulicho nacho, ili mtu asije akaichukua taji yako.
Revelation 3:11 in English
Revelation 3:11 · Berean Standard Bible
I am coming soon.* Hold fast to what you have, so that no one will take your crown.
Context
9Nitawafanya wale wa sinagogi la Shetani, wale ambao husema kuwa ni Wayahudi lakini sio, bali ni waongo, nitawafanya waje wapige magoti miguuni pako, na wakiri ya kwamba nimekupenda. 10Kwa kuwa umeshika amri yangu ya kuvumilia katika saburi, nitakulinda katika saa ya kujaribiwa inayokuja ulimwenguni pote, ili kuwajaribu wote wakaao duniani. 11“Ninakuja upesi. Shika sana ulicho nacho, ili mtu asije akaichukua taji yako. 12Yeye ashindaye nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo kamwe. Nitaandika juu yake Jina la Mungu wangu na jina la mji mkubwa wa Mungu wangu, Yerusalemu mpya, ambao unashuka kutoka mbinguni kwa Mungu wangu. Nami pia nitaandika juu yake Jina langu jipya. 13Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho ayaambia makanisa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.