Ufunuo 21:18
Revelation 21:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ukuta huo ulijengwa kwa yaspi hali mji wenyewe ulijengwa kwa dhahabu safi, ikingʼaa kama kioo.
Revelation 21:18 in English
Revelation 21:18 · Berean Standard Bible
The wall was made of jasper, and the city itself of pure gold, as pure as glass.
Context
16Mji huo ulikuwa mraba, urefu wake ulikuwa sawa na upana wake. Akaupima huo mji kwa huo ufito akakuta una kama kilomita 2,200;* urefu wake na upana wake na kwenda juu kwake vilikuwa sawa. 17Akaupima ukuta wake, ulikuwa na unene wa dhiraa 144* kwa kipimo cha kibinadamu ambacho huyo malaika alikuwa akikitumia. 18Ukuta huo ulijengwa kwa yaspi hali mji wenyewe ulijengwa kwa dhahabu safi, ikingʼaa kama kioo. 19Misingi ya kuta za mji huo zilipambwa kwa kila aina ya kito cha thamani. Msingi wa kwanza ulikuwa wa yaspi, wa pili yakuti samawi, wa tatu kalkedoni, wa nne zumaridi, 20wa tano sardoniki, wa sita akiki, wa saba krisolitho, wa nane zabarajadi, wa tisa yakuti manjano, wa kumi krisopraso, wa kumi na moja hiakintho, wa kumi na mbili amethisto.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.