Ufunuo 21:16
Revelation 21:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mji huo ulikuwa mraba, urefu wake ulikuwa sawa na upana wake. Akaupima huo mji kwa huo ufito akakuta una kama kilomita 2,200;* urefu wake na upana wake na kwenda juu kwake vilikuwa sawa.
Revelation 21:16 in English
Revelation 21:16 · Berean Standard Bible
The city lies foursquare, with its width the same as its length. And he measured the city with the rod, and all its dimensions were equal—12,000 stadia * in length and width and height.
Context
14Ukuta wa huo mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na juu yake yaliandikwa majina ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo. 15Huyo malaika aliyesema nami alikuwa na ufito wa dhahabu wa kupimia huo mji, malango yake na kuta zake. 16Mji huo ulikuwa mraba, urefu wake ulikuwa sawa na upana wake. Akaupima huo mji kwa huo ufito akakuta una kama kilomita 2,200;* urefu wake na upana wake na kwenda juu kwake vilikuwa sawa. 17Akaupima ukuta wake, ulikuwa na unene wa dhiraa 144* kwa kipimo cha kibinadamu ambacho huyo malaika alikuwa akikitumia. 18Ukuta huo ulijengwa kwa yaspi hali mji wenyewe ulijengwa kwa dhahabu safi, ikingʼaa kama kioo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.