Native Bible

Revelation 2:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Umevumilia na kustahimili taabu kwa ajili ya Jina langu, wala hukuchoka.

Revelation 2:3 in English

Revelation 2:3 · Berean Standard Bible

Without growing weary, you have persevered and endured many things for the sake of My name.

Context

1“Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika: “Haya ndiyo maneno ya yule aliyezishika zile nyota saba katika mkono wake wa kuume na ambaye hutembea kati ya vile vinara saba vya taa vya dhahabu. 2Nayajua matendo yako, bidii yako na saburi yako. Najua kuwa huwezi kuvumiliana na watu waovu na ya kwamba umewajaribu wale wanaojifanya kuwa mitume na kumbe sio, nawe umewatambua kuwa ni waongo. 3Umevumilia na kustahimili taabu kwa ajili ya Jina langu, wala hukuchoka. 4“Lakini nina neno dhidi yako: Umeuacha upendo wako wa kwanza. 5Kumbuka basi ni wapi ulikoangukia! Tubu na ukafanye matendo yale ya kwanza. Kama usipotubu, nitakuja kwako na kukiondoa kinara chako cha taa kutoka mahali pake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.