Ufunuo 18:2
Revelation 18:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Naye akalia kwa nguvu kwa sauti kubwa, akisema: “Umeanguka! Umeanguka Babeli Mkuu! Umekuwa makao ya mashetani na makazi ya kila pepo mchafu, makazi ya kila ndege na kila mnyama achukizaye.
Revelation 18:2 in English
Revelation 18:2 · Berean Standard Bible
And he cried out in a mighty voice: “Fallen, fallen is Babylon the great!* She has become a lair for demons and a haunt for every unclean spirit, every unclean bird, and every detestable beast.*
Context
1Baada ya haya nikaona malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni, akiwa na mamlaka makuu na dunia ikamulikiwa na mngʼao wake. 2Naye akalia kwa nguvu kwa sauti kubwa, akisema:
“Umeanguka! Umeanguka Babeli Mkuu!
Umekuwa makao ya mashetani
na makazi ya kila pepo mchafu,
makazi ya kila ndege na kila mnyama achukizaye. 3Kwa maana mataifa yote yamekunywa
mvinyo wa ghadhabu ya uasherati wake.
Nao wafalme wa dunia wamefanya uzinzi nao,
nao wafanyabiashara wa dunia
wametajirika kutokana na wingi wa utajiri wake.” 4Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema:
“Tokeni katikati yake, enyi watu wangu,
ili msije mkashiriki dhambi zake,
ili msije mkapatwa na pigo lake lolote;
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.