Ufunuo 16:4
Revelation 16:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Malaika wa tatu akalimwaga bakuli lake katika mito na chemchemi za maji, nazo zikawa damu.
Revelation 16:4 in English
Revelation 16:4 · Berean Standard Bible
And the third angel poured out his bowl into the rivers and springs of water, and they turned to blood.
Context
2Malaika wa kwanza akaenda akalimwaga hilo bakuli lake juu ya nchi. Majipu mabaya yenye maumivu makali yakawapata wale watu wote waliokuwa na chapa ya yule mnyama na walioabudu sanamu yake. 3Malaika wa pili akalimwaga bakuli lake baharini, nayo ikabadilika kuwa damu kama ya mtu aliyekufa na kila kiumbe hai kilichokuwa ndani ya bahari kikafa. 4Malaika wa tatu akalimwaga bakuli lake katika mito na chemchemi za maji, nazo zikawa damu. 5Ndipo nikamsikia malaika msimamizi wa maji akisema:
“Wewe una haki katika hukumu hizi ulizotoa,
wewe uliyeko, uliyekuwako, Uliye Mtakatifu,
kwa sababu umehukumu hivyo; 6kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu wako
na manabii wako,
nawe umewapa damu wanywe
kama walivyostahili.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.