Ufunuo 12:11
Revelation 12:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo na kwa neno la ushuhuda wao. Wala wao hawakuyapenda maisha yao hata kufa.
Revelation 12:11 in English
Revelation 12:11 · Berean Standard Bible
They have conquered him by the blood of the Lamb and by the word of their testimony. And they did not love their lives so as to shy away from death.
Context
9Lile joka kuu likatupwa chini, yule nyoka wa zamani aitwaye ibilisi au Shetani, aupotoshaye ulimwengu wote. Akatupwa chini duniani, yeye pamoja na malaika zake. 10Kisha nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema:
“Sasa wokovu na uweza na Ufalme wa Mungu wetu umekuja
na mamlaka ya Kristo wake.
Kwa kuwa ametupwa chini
mshtaki wa ndugu zetu,
anayewashtaki mbele za Mungu
usiku na mchana. 11Nao wakamshinda
kwa damu ya Mwana-Kondoo
na kwa neno la ushuhuda wao.
Wala wao hawakuyapenda maisha yao
hata kufa. 12Kwa hiyo, furahini ninyi mbingu
na wote wakaao humo!
Lakini ole wenu nchi na bahari,
kwa maana huyo ibilisi ameshuka kwenu,
akiwa amejaa ghadhabu,
kwa sababu anajua ya kuwa
muda wake ni mfupi!” 13Lile joka lilipoona kuwa limetupwa chini duniani, lilimfuatilia yule mwanamke aliyekuwa amezaa mtoto mwanaume.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.