Native Bible

Psalms 96:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi; bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake;

Psalms 96:11 in English

Psalms 96:11 · Berean Standard Bible

Let the heavens be glad and the earth rejoice; let the sea resound, and all that fills it.

Context

9Mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake; dunia yote na itetemeke mbele zake. 10Katikati ya mataifa semeni, “Bwana anatawala.” Ulimwengu ameuweka imara, hauwezi kusogezwa; atawahukumu watu kwa uadilifu. 11Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi; bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake; 12mashamba na yashangilie, pamoja na vyote vilivyomo ndani yake. Kisha miti yote ya msituni itaimba kwa furaha; 13itaimba mbele za Bwana kwa maana anakuja, anakuja kuihukumu dunia. Ataihukumu dunia kwa haki, na mataifa katika kweli yake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.