Zaburi 79:3
Psalms 79:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wamemwaga damu kama maji kuzunguka Yerusalemu yote, wala hakuna yeyote wa kuwazika.
Psalms 79:3 in English
Psalms 79:3 · Berean Standard Bible
They have poured out their blood like water all around Jerusalem, and there is no one to bury the dead.
Context
1Ee Mungu, mataifa yameuvamia urithi wako,
wamelinajisi Hekalu lako takatifu,
wameifanya Yerusalemu kuwa magofu. 2Wametoa maiti za watumishi
kuwa chakula cha ndege wa angani
na nyama ya watakatifu wako
kwa wanyama wa nchi. 3Wamemwaga damu kama maji
kuzunguka Yerusalemu yote,
wala hakuna yeyote wa kuwazika. 4Tumekuwa kitu cha aibu kwa jirani zetu,
cha dharau na mzaha kwa wale wanaotuzunguka. 5Hata lini, Ee Bwana? Je, wewe utakasirika milele?
Wivu wako utawaka kama moto hadi lini?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.