Native Bible

Psalms 59:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini usiwaue, Ee Bwana, ngao yetu, au sivyo watu wangu watasahau. Katika uwezo wako wafanye watangetange na uwashushe chini.

Psalms 59:11 in English

Psalms 59:11 · Berean Standard Bible

Do not kill them, or my people will forget. Scatter them by Your power, and bring them down, O Lord, our shield.

Context

9Ee nguvu yangu, ninakutazama wewe, wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu, 10Mungu wangu unipendaye. Mungu atanitangulia, naye atanifanya niwachekelee wale wanaonisingizia. 11Lakini usiwaue, Ee Bwana, ngao yetu, au sivyo watu wangu watasahau. Katika uwezo wako wafanye watangetange na uwashushe chini. 12Kwa ajili ya dhambi za vinywa vyao, kwa ajili ya maneno ya midomo yao, waache wanaswe katika kiburi chao. Kwa ajili ya laana na uongo wanaotamka, 13wateketeze katika ghadhabu, wateketeze hadi wasiwepo tena. Ndipo itakapofahamika katika miisho ya dunia kwamba Mungu anatawala juu ya Yakobo.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.