Zaburi 53:3
Psalms 53:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kila mmoja amegeukia mbali, wameharibika wote pamoja, hakuna atendaye mema. Naam, hakuna hata mmoja!
Psalms 53:3 in English
Psalms 53:3 · Berean Standard Bible
All have turned away, they have together become corrupt;* there is no one who does good, not even one.*
Context
1Mpumbavu anasema moyoni mwake,
“Hakuna Mungu.”
Wameharibika, na njia zao ni za uovu kabisa,
hakuna hata mmoja atendaye mema. 2Mungu anawachungulia wanadamu chini
kutoka mbinguni
aone kama wako wenye akili,
wowote wanaomtafuta Mungu. 3Kila mmoja amegeukia mbali,
wameharibika wote pamoja,
hakuna atendaye mema.
Naam, hakuna hata mmoja! 4Je, watendao mabaya kamwe hawatajifunza:
wale ambao huwala watu wangu
kama watu walavyo mkate,
hao ambao hawamwiti Mungu? 5Hapo waliingiwa na hofu kuu,
ambapo hapakuwa cha kutetemesha.
Mungu alitawanya mifupa ya wale waliokushambulia;
uliwaaibisha, kwa sababu Mungu aliwadharau.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.