Zaburi 44:2
Psalms 44:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa mkono wako uliwafukuza mataifa na ukawapanda baba zetu, uliangamiza mataifa na kuwastawisha baba zetu.
Psalms 44:2 in English
Psalms 44:2 · Berean Standard Bible
With Your hand You drove out the nations and planted our fathers there; You crushed the peoples and cast them out.
Context
1Ee Mungu, tumesikia kwa masikio yetu,
baba zetu wametueleza
yale uliyotenda katika siku zao,
siku za kale. 2Kwa mkono wako uliwafukuza mataifa
na ukawapanda baba zetu,
uliangamiza mataifa
na kuwastawisha baba zetu. 3Sio kwa upanga wao waliipata nchi,
wala si mkono wao uliwapatia ushindi;
ilikuwa ni kitanga cha mkono wako wa kuume,
na nuru ya uso wako,
kwa kuwa uliwapenda. 4Wewe ni mfalme wangu na Mungu wangu,
unayeamuru ushindi kwa Yakobo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.