Zaburi 44:16
Psalms 44:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
kwa ajili ya dhihaka ya wale wanaonilaumu na kunitukana, kwa sababu ya adui, ambaye anatamani kulipiza kisasi.
Psalms 44:16 in English
Psalms 44:16 · Berean Standard Bible
at the voice of the scorner and reviler, because of the enemy, bent on revenge.
Context
14Umetufanya kuwa mithali miongoni mwa mataifa,
mataifa hutikisa vichwa vyao. 15Fedheha yangu iko mbele yangu mchana kutwa,
na uso wangu umejaa aibu tele, 16kwa ajili ya dhihaka ya wale wanaonilaumu na kunitukana,
kwa sababu ya adui, ambaye anatamani kulipiza kisasi. 17Hayo yote yametutokea,
ingawa tulikuwa hatujakusahau
wala hatujaenda kinyume na agano lako. 18Mioyo yetu ilikuwa haijarudi nyuma;
nyayo zetu zilikuwa hazijaiacha njia yako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.