Zaburi 28:2
Psalms 28:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sikia kilio changu unihurumie ninapokuita kwa ajili ya msaada, niinuapo mikono yangu kuelekea Patakatifu pa Patakatifu pako.
Psalms 28:2 in English
Psalms 28:2 · Berean Standard Bible
Hear my cry for mercy when I call to You for help, when I lift up my hands toward Your holy sanctuary.*
Context
1Ninakuita wewe, Ee Bwana, Mwamba wangu;
usiwe kwangu kama kiziwi.
Kwa sababu ukinyamaza
nitafanana na walioshuka shimoni. 2Sikia kilio changu unihurumie
ninapokuita kwa ajili ya msaada,
niinuapo mikono yangu kuelekea
Patakatifu pa Patakatifu pako. 3Usiniburute pamoja na waovu,
pamoja na hao watendao mabaya,
ambao huzungumza na jirani zao maneno mazuri,
lakini mioyoni mwao wameficha chuki. 4Walipe sawasawa na matendo yao,
sawasawa na matendo yao maovu;
walipe sawasawa na kazi za mikono yao,
uwalipe wanavyostahili.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.