Native Bible

Psalms 18:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Alinyoosha mkono kutoka juu na kunishika; alinitoa kutoka kilindi cha maji makuu.

Psalms 18:16 in English

Psalms 18:16 · Berean Standard Bible

He reached down from on high and took hold of me; He drew me out of deep waters.

Context

14Aliipiga mishale yake na kutawanya adui, naam, umeme mwingi wa radi na kuwafukuza. 15Mabonde ya bahari yalifunuliwa, na misingi ya dunia ikawa wazi kwa kukaripia kwako, Ee Bwana, kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwako. 16Alinyoosha mkono kutoka juu na kunishika; alinitoa kutoka kilindi cha maji makuu. 17Aliniokoa kutoka adui wangu mwenye nguvu nyingi, kutoka adui zangu waliokuwa na nguvu nyingi kuliko mimi. 18Walinikabili siku ya msiba wangu, lakini Bwana alikuwa msaada wangu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.