Zaburi 143:9
Psalms 143:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ee Bwana, uniokoe na adui zangu, kwa kuwa nimejificha kwako.
Psalms 143:9 in English
Psalms 143:9 · Berean Standard Bible
Deliver me from my enemies, O LORD; I flee to You for refuge.*
Context
7Ee Bwana, unijibu haraka,
roho yangu inazimia.
Usinifiche uso wako,
ama sivyo nitafanana na wale washukao shimoni. 8Asubuhi uniletee neno la upendo wako usiokoma,
kwa kuwa nimeweka tumaini langu kwako.
Nionyeshe njia nitakayoiendea,
kwa kuwa kwako nainua nafsi yangu. 9Ee Bwana, uniokoe na adui zangu,
kwa kuwa nimejificha kwako. 10Nifundishe kufanya mapenzi yako,
kwa maana wewe ndiwe Mungu wangu,
Roho wako mwema na aniongoze
katika nchi tambarare. 11Ee Bwana, kwa ajili ya jina lako, hifadhi maisha yangu,
kwa haki yako nitoe katika taabu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.