Zaburi 14:3
Psalms 14:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wote wamepotoka, wameharibika wote pamoja, hakuna atendaye mema. Naam, hakuna hata mmoja!
Psalms 14:3 in English
Psalms 14:3 · Berean Standard Bible
All have turned away, they have together become corrupt;* there is no one who does good, not even one.*
Context
1Mpumbavu anasema moyoni mwake,
“Hakuna Mungu.”
Wameharibika, matendo yao ni maovu kabisa;
hakuna hata mmoja atendaye mema. 2Bwana anawachungulia wanadamu chini
kutoka mbinguni
aone kama wako wenye akili,
wowote wanaomtafuta Mungu. 3Wote wamepotoka,
wameharibika wote pamoja,
hakuna atendaye mema.
Naam, hakuna hata mmoja! 4Je, watendao mabaya kamwe hawatajifunza:
wale ambao huwala watu wangu
kama watu walavyo mkate,
hao ambao hawamwiti Bwana? 5Wako hapo, wameingiwa na hofu kuu,
maana Mungu yupo pamoja na wenye haki.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.