Zaburi 106:30
Psalms 106:30 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini Finehasi alisimama na kuingilia kati, nayo tauni ikazuiliwa.
Psalms 106:30 in English
Psalms 106:30 · Berean Standard Bible
But Phinehas stood and intervened, and the plague was restrained.
Context
28Walijifunga nira na Baali wa Peori,
wakala dhabihu zilizotolewa kwa miungu isiyo na uhai. 29Waliichochea hasira ya Bwana,
wakamkasirisha kwa matendo yao maovu,
nayo tauni ikazuka katikati yao. 30Lakini Finehasi alisimama na kuingilia kati,
nayo tauni ikazuiliwa. 31Hili likahesabiwa kwake haki,
kwa vizazi visivyo na mwisho vijavyo. 32Kwenye maji ya Meriba, walimkasirisha Bwana,
janga likampata Mose kwa sababu yao;
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.