Zaburi 1:3
Psalms 1:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mtu huyo ni kama mti uliopandwa kando ya vijito vya maji, ambao huzaa matunda kwa majira yake na majani yake hayanyauki. Lolote afanyalo hufanikiwa.
Psalms 1:3 in English
Psalms 1:3 · Berean Standard Bible
He is like a tree planted by streams of water, yielding its fruit in season, whose leaf does not wither, and who prospers in all he does.
Context
1Heri mtu yule ambaye
haendi katika shauri la watu waovu,
wala hasimami katika njia ya wenye dhambi,
au kuketi katika baraza la wenye mizaha. 2Bali huifurahia sheria ya Bwana,
naye huitafakari hiyo sheria usiku na mchana. 3Mtu huyo ni kama mti uliopandwa
kando ya vijito vya maji,
ambao huzaa matunda kwa majira yake
na majani yake hayanyauki.
Lolote afanyalo hufanikiwa. 4Sivyo walivyo waovu!
Wao ni kama makapi
yapeperushwayo na upepo. 5Kwa hiyo waovu hawatastahimili hukumu,
wala wenye dhambi katika kusanyiko la wenye haki.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.