Mithali 28:17
Proverbs 28:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mtu mwenye kusumbuliwa na hatia ya kuua atakuwa mtoro mpaka kufa; mtu yeyote na asimsaidie.
Proverbs 28:17 in English
Proverbs 28:17 · Berean Standard Bible
A man burdened by bloodguilt will flee into the Pit;* let no one support him.
Context
15Kama simba angurumaye au dubu ashambuliaye,
ndivyo alivyo mtu mwovu atawalaye wanyonge. 16Mtawala dhalimu hana akili,
bali yeye achukiaye mapato ya udhalimu
atafurahia maisha marefu. 17Mtu mwenye kusumbuliwa na hatia ya kuua
atakuwa mtoro mpaka kufa;
mtu yeyote na asimsaidie. 18Yeye ambaye mwenendo wake hauna lawama
hulindwa salama,
bali yeye ambaye njia zake ni potovu
ataanguka ghafula. 19Yeye alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele,
bali yule afuataye mambo ya upuzi atakuwa na umaskini wa kumtosha.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.