Mithali 15:7
Proverbs 15:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Midomo ya mwenye hekima hueneza maarifa, bali sivyo ilivyo mioyo ya wapumbavu.
Proverbs 15:7 in English
Proverbs 15:7 · Berean Standard Bible
The lips of the wise spread knowledge, but not so the hearts of fools.
Context
5Mpumbavu hubeza maonyo ya baba yake,
bali yeyote akubaliye maonyo huonyesha busara. 6Nyumba ya mwenye haki ina hazina kubwa,
bali mapato ya waovu huwaletea taabu. 7Midomo ya mwenye hekima hueneza maarifa,
bali sivyo ilivyo mioyo ya wapumbavu. 8Bwana huchukia sana dhabihu za waovu,
bali maombi ya wanyofu humfurahisha Mungu. 9Bwana huchukia sana njia ya waovu,
bali huwapenda wale wafuatao haki.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.