Wafilipi 4:6
Philippians 4:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Msijisumbue kwa jambo lolote, bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
Philippians 4:6 in English
Philippians 4:6 · Berean Standard Bible
Be anxious for nothing, but in everything, by prayer and petition, with thanksgiving, present your requests to God.
Context
4Furahini katika Bwana siku zote, tena nasema furahini! 5Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu. 6Msijisumbue kwa jambo lolote, bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. 7Nayo amani ya Mungu, inayopita fahamu zote, itailinda mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu. 8Hatimaye, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo na sifa njema, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote ya kupendeza, yoyote yenye staha, ukiwepo uzuri wowote, pakiwepo chochote kinachostahili kusifiwa, tafakarini mambo hayo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.