Native Bible

Philippians 2:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nami mwenyewe ninatumaini katika Bwana kwamba nitakuja kwenu hivi karibuni.

Philippians 2:24 in English

Philippians 2:24 · Berean Standard Bible

And I trust in the Lord that I myself will come soon.

Context

22Lakini ninyi wenyewe mnajua jinsi Timotheo alivyojithibitisha mwenyewe, kwa maana ametumika pamoja nami kwa kazi ya Injili, kama vile mwana kwa baba yake. 23Kwa hiyo, ninatumaini kumtuma kwenu upesi mara nitakapojua mambo yangu yatakavyokuwa. 24Nami mwenyewe ninatumaini katika Bwana kwamba nitakuja kwenu hivi karibuni. 25Lakini nadhani ni muhimu kumtuma tena kwenu Epafrodito, ndugu yangu na mtendakazi pamoja nami, aliye askari mwenzangu, ambaye pia ni mjumbe wenu mliyemtuma ili ashughulike na mahitaji yangu. 26Kwa maana amekuwa akiwaonea sana shauku ninyi nyote, akiwa na wasiwasi kwa kuwa mlisikia kwamba alikuwa mgonjwa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.