Hesabu 6:5
Numbers 6:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“ ‘Kwa muda wote wa nadhiri yake ya kujitenga kwa ajili ya Bwana, wembe hautapita kichwani mwake. Ni lazima awe mtakatifu mpaka kipindi cha kujitenga kwake kwa ajili ya Bwana kiishe; ni lazima aache nywele za kichwa chake zirefuke.
Numbers 6:5 in English
Numbers 6:5 · Berean Standard Bible
For the entire period of his vow of separation, no razor shall pass over his head. He must be holy until the time of his separation to the LORD is complete; he must let the hair of his head grow long.
Context
3ni lazima ajitenge na mvinyo na kinywaji kingine chochote chenye chachu, na kamwe asinywe siki itokanayo na mvinyo au itokanayo na kinywaji kingine chenye chachu. Kamwe asinywe maji ya zabibu wala kula zabibu mbichi au kavu. 4Kwa muda wote atakaokuwa Mnadhiri, kamwe hatakula chochote kitokanacho na mzabibu, sio mbegu wala maganda. 5“ ‘Kwa muda wote wa nadhiri yake ya kujitenga kwa ajili ya Bwana, wembe hautapita kichwani mwake. Ni lazima awe mtakatifu mpaka kipindi cha kujitenga kwake kwa ajili ya Bwana kiishe; ni lazima aache nywele za kichwa chake zirefuke. 6Kwa kipindi chochote cha kujitenga kwa ajili ya Bwana hatakaribia maiti. 7Hata kama baba yake mwenyewe au mama au kaka au dada akifa, hatajinajisi mwenyewe kwa taratibu za ibada kwa ajili yao, kwa sababu ishara ya kujiweka wakfu kwake kwa Mungu ipo katika kichwa chake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.