Hesabu 32:31
Numbers 32:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wagadi na Wareubeni wakajibu, “Watumishi wako watafanya lile Bwana alilosema.
Numbers 32:31 in English
Numbers 32:31 · Berean Standard Bible
The Gadites and Reubenites replied, “As the LORD has spoken to your servants, so we will do.
Context
29Mose akawaambia, “Ikiwa Wagadi na Wareubeni, kila mwanaume aliyevaa silaha za vita, atavuka Yordani pamoja nanyi mbele za Bwana, basi wakati mtakapoishinda nchi iliyoko mbele yenu, wapeni nchi ya Gileadi kama milki yao. 30Lakini kama hawatavuka pamoja nanyi wakiwa wamevaa silaha za vita, lazima wakubali kupokea milki yao pamoja nanyi katika nchi ya Kanaani.” 31Wagadi na Wareubeni wakajibu, “Watumishi wako watafanya lile Bwana alilosema. 32Tutavuka mbele za Bwana kuingia Kanaani tukiwa tumevaa silaha za vita, lakini mali tutakayoirithi itakuwa ngʼambo hii ya Yordani.” 33Kisha Mose akawapa Wagadi, Wareubeni, na nusu ya kabila la Manase mwana wa Yosefu ufalme wa Sihoni mfalme wa Waamori, na ufalme wa Ogu mfalme wa Bashani, nchi yote pamoja na miji yake, na nchi inayowazunguka.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.