Hesabu 32:10
Numbers 32:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Siku ile hasira ya Bwana iliwaka naye akaapa kiapo hiki:
Numbers 32:10 in English
Numbers 32:10 · Berean Standard Bible
So the anger of the LORD was kindled that day, and He swore an oath, saying,
Context
8Hivi ndivyo baba zenu walivyofanya wakati nilipowatuma kutoka Kadesh-Barnea kuipeleleza nchi. 9Baada ya kufika kwenye Bonde la Eshkoli na kuitazama nchi, waliwakatisha tamaa Waisraeli wasiingie katika nchi ambayo Bwana alikuwa amewapa. 10Siku ile hasira ya Bwana iliwaka naye akaapa kiapo hiki: 11‘Kwa kuwa hawakunifuata kwa moyo wote, hakuna mtu yeyote mwenye miaka ishirini au zaidi ambaye alikuja kutoka Misri atakayeona nchi niliyoahidi kwa kiapo kwa Abrahamu, Isaki na Yakobo; 12hakuna hata mmoja isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, Mkenizi, na Yoshua mwana wa Nuni, kwa sababu walimfuata Bwana kwa moyo wote.’
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.