Native Bible

Numbers 3:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Walete watu wa kabila la Lawi mbele ya Aroni kuhani ili wamsaidie.

Numbers 3:6 in English

Numbers 3:6 · Berean Standard Bible

“Bring the tribe of Levi and present them to Aaron the priest to assist him.

Context

4Hata hivyo Nadabu na Abihu walikufa mbele za Bwana walipotoa sadaka kwa moto usioruhusiwa mbele zake katika Jangwa la Sinai. Hawakuwa na wana; kwa hiyo Eleazari na Ithamari walihudumu peke yao kama makuhani wakati wote wa maisha ya Aroni baba yao. 5Bwana akamwambia Mose, 6“Walete watu wa kabila la Lawi mbele ya Aroni kuhani ili wamsaidie. 7Watafanya huduma kwa ajili yake na kwa jumuiya yote katika Hema la Kukutania kwa kufanya kazi za Maskani. 8Watatunza samani zote za Hema la Kukutania, wakitimiza wajibu wa kuhudumia Waisraeli kwa kufanya kazi ya Maskani.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.