Native Bible

Numbers 28:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Pamoja na kila fahali kutakuwa na sadaka ya kinywaji nusu ya hini* ya divai; pamoja na kila kondoo dume, theluthi moja ya hini,* na pamoja na kila mwana-kondoo robo hini. Hii ni sadaka ya kuteketezwa ya kila mwezi itakayotolewa kila mwandamo wa mwezi kwa mwaka.

Numbers 28:14 in English

Numbers 28:14 · Berean Standard Bible

Their drink offerings shall be half a hin of wine * with each bull, a third of a hin * with the ram, and a quarter hin with each lamb. This is the monthly burnt offering to be made at each new moon throughout the year.

Context

12Pamoja na kila fahali, kutakuwa na sadaka ya nafaka ya unga laini sehemu tatu za kumi za efa,* uliochanganywa na mafuta, pamoja na kondoo dume mmoja, sadaka ya nafaka ya unga laini uliochanganywa na mafuta; 13pamoja na kila mwana-kondoo, sadaka ya nafaka yenye uzito wa sehemu ya kumi ya efa ya unga laini uliochanganywa na mafuta. Hii ni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, harufu nzuri, sadaka ya kuteketezwa iliyotolewa kwa moto kwa Bwana. 14Pamoja na kila fahali kutakuwa na sadaka ya kinywaji nusu ya hini* ya divai; pamoja na kila kondoo dume, theluthi moja ya hini,* na pamoja na kila mwana-kondoo robo hini. Hii ni sadaka ya kuteketezwa ya kila mwezi itakayotolewa kila mwandamo wa mwezi kwa mwaka. 15Zaidi ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya kinywaji, mbuzi mmoja dume atatolewa kwa Bwana kama sadaka ya dhambi. 16“ ‘Katika siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza, itafanyika Pasaka ya Bwana.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.