Hesabu 27:20
Numbers 27:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mpe sehemu ya mamlaka yako ili jumuiya yote ya Waisraeli ipate kumtii.
Numbers 27:20 in English
Numbers 27:20 · Berean Standard Bible
Confer on him some of your authority, so that the whole congregation of Israel will obey him.
Context
18Kwa hiyo Bwana akamwambia Mose, “Mchukue Yoshua mwana wa Nuni, mtu ambaye Roho yuko ndani yake, uweke mkono juu yake. 19Msimamishe mbele ya kuhani Eleazari pamoja na kusanyiko lote, umpe maagizo mbele yao. 20Mpe sehemu ya mamlaka yako ili jumuiya yote ya Waisraeli ipate kumtii. 21Atasimama mbele ya kuhani Eleazari, ambaye atapokea maamuzi kwa ajili yake, kwa kuuliza mbele za Bwana kwa ile Urimu.* Kwa amri yake, yeye na jumuiya yote ya Waisraeli watatoka, na kwa amri yake, wataingia.” 22Mose akafanya kama Bwana alivyomwagiza. Akamtwaa Yoshua na kumsimamisha mbele ya kuhani Eleazari na kusanyiko lote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.