Hesabu 24:11
Numbers 24:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sasa ondoka upesi uende nyumbani! Mimi nilisema nitakuzawadia vizuri sana, lakini Bwana amekuzuia usizawadiwe.”
Numbers 24:11 in English
Numbers 24:11 · Berean Standard Bible
Therefore, flee at once to your home! I said I would richly reward you, but instead the LORD has denied your reward.”
Context
9Hujikunyata na kuvizia kama simba,
kama simba jike; nani anayethubutu kumwamsha?
“Abarikiwe kila akubarikiye,
na alaaniwe kila akulaaniye!” 10Ndipo hasira ya Balaki ikawaka dhidi ya Balaamu. Akapiga mikono yake pamoja, akamwambia Balaamu, “Nilikuita uje kuwalaani adui zangu, lakini umewabariki mara hizi tatu. 11Sasa ondoka upesi uende nyumbani! Mimi nilisema nitakuzawadia vizuri sana, lakini Bwana amekuzuia usizawadiwe.” 12Balaamu akamwambia Balaki, “Je, hukumbuki jinsi nilivyowaambia wajumbe uliowatuma kwangu? Niliwaambia hivi, 13‘Hata ikiwa Balaki angenipa jumba lake la kifalme likiwa limejazwa fedha na dhahabu, nisingeweza kufanya kitu chochote kwa matakwa yangu, kikiwa kizuri au kibaya, kwenda kinyume na agizo la Bwana, nami imenipasa kusema tu kile Bwana atakachosema’?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.