Hesabu 23:9
Numbers 23:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kutoka vilele vya miamba ninawaona, kutoka mahali palipoinuka ninawatazama. Ninaliona taifa ambalo wanaishi peke yao, nao hawahesabiwi kama mojawapo ya mataifa.
Numbers 23:9 in English
Numbers 23:9 · Berean Standard Bible
For I see them from atop the rocky cliffs, and I watch them from the hills. Behold, a people dwelling apart, not reckoning themselves among the nations.
Context
7Ndipo Balaamu akasema ujumbe wake:
“Balaki amenileta kutoka Aramu,
mfalme wa Moabu kutoka milima ya mashariki.
Akasema, ‘Njoo, unilaanie Yakobo;
njoo unishutumie Israeli.’ 8Nitawezaje kuwalaani,
hao ambao Mungu hajawalaani?
Nitawezaje kuwashutumu
hao ambao Bwana hakuwashutumu? 9Kutoka vilele vya miamba ninawaona,
kutoka mahali palipoinuka ninawatazama.
Ninaliona taifa ambalo wanaishi peke yao,
nao hawahesabiwi kama mojawapo ya mataifa. 10Ni nani awezaye kuhesabu mavumbi ya Yakobo,
au kuhesabu robo ya Israeli?
Mimi na nife kifo cha mtu mwenye haki,
na mwisho wangu na uwe kama wao!” 11Balaki akamwambia Balaamu, “Ni nini ulichonitendea? Nimekuleta ulaani adui zangu, lakini wewe badala yake umewabariki!”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.