Hesabu 23:5
Numbers 23:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bwana akaweka ujumbe katika kinywa cha Balaamu na kusema, “Rudi kwa Balaki umpe ujumbe huu.”
Numbers 23:5 in English
Numbers 23:5 · Berean Standard Bible
Then the LORD put a message in Balaam’s mouth, saying, “Return to Balak and give him this message.”
Context
3Kisha Balaamu akamwambia Balaki, “Kaa hapa kando ya sadaka yako wakati mimi ninakwenda kando. Huenda Bwana atakuja kukutana nami. Lolote atakalonifunulia, nitakuambia.” Basi akaenda hata mahali peupe palipoinuka. 4Mungu akakutana naye, kisha Balaamu akasema, “Nimekwisha kutengeneza madhabahu saba, na juu ya kila madhabahu nimetoa sadaka ya fahali mmoja na kondoo dume mmoja.” 5Bwana akaweka ujumbe katika kinywa cha Balaamu na kusema, “Rudi kwa Balaki umpe ujumbe huu.” 6Basi Balaamu akarudi kwa Balaki, akamkuta amesimama kando ya sadaka yake akiwa na wakuu wote wa Moabu. 7Ndipo Balaamu akasema ujumbe wake:
“Balaki amenileta kutoka Aramu,
mfalme wa Moabu kutoka milima ya mashariki.
Akasema, ‘Njoo, unilaanie Yakobo;
njoo unishutumie Israeli.’
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.