Native Bible

Numbers 21:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ndipo Bwana akapeleka nyoka wenye sumu katikati yao; wakawauma watu, nao Waisraeli wengi wakafa.

Numbers 21:6 in English

Numbers 21:6 · Berean Standard Bible

So the LORD sent venomous snakes among the people, and many of the Israelites were bitten and died.

Context

4Waisraeli wakasafiri kutoka mlima Hori kupitia njia inayoelekea Bahari ya Shamu,* kuizunguka Edomu. Lakini watu wakakosa uvumilivu njiani, 5wakamnungʼunikia Mungu na Mose, wakisema, “Kwa nini umetupandisha kutoka Misri ili tufe jangwani? Hakuna mkate! Hakuna maji! Nasi tunachukia sana chakula hiki duni!” 6Ndipo Bwana akapeleka nyoka wenye sumu katikati yao; wakawauma watu, nao Waisraeli wengi wakafa. 7Watu wakamjia Mose na kusema, “Tumetenda dhambi wakati tuliponena dhidi ya Bwana na dhidi yako. Mwombe Bwana ili atuondolee hawa nyoka.” Hivyo Mose akawaombea hao watu. 8Bwana akamwambia Mose, “Tengeneza nyoka wa shaba na umweke juu ya mti; yeyote aliyeumwa na nyoka anaweza kumtazama na akaishi tena.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.