Native Bible

Numbers 21:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Waisraeli wakasafiri kutoka mlima Hori kupitia njia inayoelekea Bahari ya Shamu,* kuizunguka Edomu. Lakini watu wakakosa uvumilivu njiani,

Numbers 21:4 in English

Numbers 21:4 · Berean Standard Bible

Then they set out from Mount Hor along the route to the Red Sea,* in order to bypass the land of Edom. But the people grew impatient on the journey

Context

2Ndipo Israeli akaweka nadhiri hii kwa Bwana: “Ikiwa utawatia watu hawa mikononi mwetu, tutaiangamiza kabisa miji yao.” 3Bwana akasikiliza ombi la Waisraeli, naye akawapa ushindi juu ya Wakanaani. Wakawaangamiza kabisa na miji yao; hivyo mahali pale pakaitwa Horma.* 4Waisraeli wakasafiri kutoka mlima Hori kupitia njia inayoelekea Bahari ya Shamu,* kuizunguka Edomu. Lakini watu wakakosa uvumilivu njiani, 5wakamnungʼunikia Mungu na Mose, wakisema, “Kwa nini umetupandisha kutoka Misri ili tufe jangwani? Hakuna mkate! Hakuna maji! Nasi tunachukia sana chakula hiki duni!” 6Ndipo Bwana akapeleka nyoka wenye sumu katikati yao; wakawauma watu, nao Waisraeli wengi wakafa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.