Native Bible

Numbers 1:49 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Kamwe usihesabu kabila la Lawi wala kuwaweka pamoja katika hesabu ya Waisraeli wengine.

Numbers 1:49 in English

Numbers 1:49 · Berean Standard Bible

“Do not number the tribe of Levi in the census with the other Israelites.

Context

47Hata hivyo, jamaa ya kabila la Lawi hawakuhesabiwa pamoja na wengine. 48Bwana alikuwa amemwambia Mose: 49“Kamwe usihesabu kabila la Lawi wala kuwaweka pamoja katika hesabu ya Waisraeli wengine. 50Badala yake, waweke Walawi kuwa viongozi wa Maskani ya Ushuhuda, juu ya samani zake na kila kitu kilichomo ndani yake. Wao watabeba Maskani na samani zake zote; wataitunza na kupiga kambi kuizunguka. 51Wakati wowote Maskani inapohamishwa, Walawi wataifungua, na wakati wowote maskani inapotakiwa kusimamishwa, Walawi watafanya kazi hiyo. Mtu yeyote mwingine ambaye atasogea karibu nayo atauawa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.