Nehemia 13:8
Nehemiah 13:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nilikasirika sana na nikavitupa nje vyombo vyote vya Tobia.
Nehemiah 13:8 in English
Nehemiah 13:8 · Berean Standard Bible
And I was greatly displeased and threw all of Tobiah’s household goods out of the room.
Context
6Lakini wakati haya yote yalipokuwa yakitendeka, sikuwa Yerusalemu, kwa kuwa katika mwaka wa thelathini na mbili wa utawala wa Artashasta mfalme wa Babeli nilikuwa nimerudi kwa mfalme. Baadaye nilimwomba ruhusa, 7nikarudi Yerusalemu. Hapo niligundua jambo la uovu alilofanya Eliashibu kwa kumpa Tobia chumba katika nyua za nyumba ya Mungu. 8Nilikasirika sana na nikavitupa nje vyombo vyote vya Tobia. 9Nilitoa amri kutakasa vyumba, kisha nikavirudisha vifaa vya nyumba ya Mungu, pamoja na sadaka za nafaka na uvumba. 10Pia niligundua kuwa mafungu yaliyopangwa kupewa Walawi hawakuwa wamepewa, nao Walawi wote na waimbaji waliowajibika kwa huduma walikuwa wamerudi katika mashamba yao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.