Nehemia 11:2
Nehemiah 11:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Watu waliwasifu wale wote waliojitolea kuishi Yerusalemu.
Nehemiah 11:2 in English
Nehemiah 11:2 · Berean Standard Bible
And the people blessed all the men who volunteered to live in Jerusalem.
Context
1Basi viongozi wa watu walikaa Yerusalemu, nao watu wale wengine walipiga kura ili kuleta mtu mmoja kati ya watu kumi aje kuishi Yerusalemu, mji mtakatifu, nao wengine tisa waliobaki wakae katika miji yao wenyewe. 2Watu waliwasifu wale wote waliojitolea kuishi Yerusalemu. 3Hawa ndio viongozi wa majimbo waliokuja kuishi Yerusalemu (baadhi ya Waisraeli, makuhani, Walawi, watumishi wa Hekalu,* na wazao wa watumishi wa Solomoni waliendelea kuishi katika miji ya Yuda, kila mmoja katika milki yake mwenyewe katika miji mbalimbali, 4ambapo watu wengine kutoka Yuda na Benyamini waliishi Yerusalemu).
Kutoka wazao wa Yuda:
Athaya mwana wa Uzia, mwana wa Zekaria, mwana wa Amaria, mwana wa Shefatia, mwana wa Mahalaleli, mzao wa Peresi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.