Native Bible

Nehemiah 10:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Tunakubali wajibu wa kutimiza amri za kutoa theluthi ya shekeli* kila mwaka kwa ajili ya utumishi wa nyumba ya Mungu:

Nehemiah 10:32 in English

Nehemiah 10:32 · Berean Standard Bible

We also place ourselves under the obligation to contribute a third of a shekel * yearly for the service of the house of our God:

Context

30“Tunaahidi kutowaoza binti zetu kwa watu wanaotuzunguka, wala kuwaoza wana wetu binti zao. 31“Wakati mataifa jirani waletapo bidhaa zao au nafaka kuuza siku ya Sabato, hatutazinunua kutoka kwao siku ya Sabato, wala siku nyingine yoyote takatifu. Kila mwaka wa saba, tutaacha kuilima ardhi na tutafuta madeni yote. 32“Tunakubali wajibu wa kutimiza amri za kutoa theluthi ya shekeli* kila mwaka kwa ajili ya utumishi wa nyumba ya Mungu: 33Kwa ajili ya mikate ya Wonyesho, kwa ajili ya sadaka za kawaida za nafaka na sadaka za kuteketezwa, kwa ajili ya sadaka za siku za Sabato, Sikukuu za Mwandamo wa Mwezi na sikukuu nyingine zilizoamriwa, kwa ajili ya sadaka takatifu, kwa ajili ya sadaka za dhambi ili kufanya upatanisho kwa ajili ya Israeli, na kwa ajili ya kazi zote za nyumba ya Mungu wetu. 34“Sisi makuhani, Walawi na watu, tumepiga kura kuamua kuwa kila mmoja wa jamaa zetu lazima alete katika nyumba ya Mungu wetu kwa nyakati maalum kila mwaka mchango wa kuni za kukokea moto katika madhabahu ya Bwana Mungu wetu, kama ilivyoandikwa katika Sheria.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.