Native Bible

Mark 7:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mara mwanamke mmoja, ambaye binti yake mdogo alikuwa na pepo mchafu, akaja na kumpigia magoti miguuni pake.

Mark 7:25 in English

Mark 7:25 · Berean Standard Bible

Instead, a woman whose little daughter had an unclean spirit soon heard about Jesus, and she came and fell at His feet.

Context

23Maovu haya yote hutoka ndani ya mtu, nayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi.” 24Ndipo Yesu akaondoka hapo akaenda sehemu za Tiro. Akaingia katika nyumba moja, naye hakutaka mtu yeyote ajue kwamba yuko humo. Lakini hakuweza kujificha. 25Mara mwanamke mmoja, ambaye binti yake mdogo alikuwa na pepo mchafu, akaja na kumpigia magoti miguuni pake. 26Basi huyo mwanamke alikuwa Myunani, aliyezaliwa Foinike ya Siria.* Akamsihi Yesu amtoe binti yake huyo pepo mchafu. 27Yesu akamwambia, “Waache watoto washibe kwanza, kwa maana si vyema kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.