Native Bible

Mark 4:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Sikilizeni! Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake.

Mark 4:3 in English

Mark 4:3 · Berean Standard Bible

“Listen! A farmer went out to sow his seed.

Context

1Yesu akaanza kufundisha tena kando ya bahari. Umati wa watu uliokuwa umekusanyika kumzunguka ulikuwa mkubwa, kiasi kwamba ilimbidi Yesu aingie kwenye mashua iliyokuwa baharini na kuketi humo, nao watu wote walikuwa ufuoni mwa bahari. 2Akawafundisha mambo mengi kwa mifano, naye katika mafundisho yake akasema: 3“Sikilizeni! Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake. 4Alipokuwa akitawanya mbegu, nyingine zilianguka kando ya njia, nao ndege wakaja na kuzila. 5Nyingine zilianguka kwenye ardhi yenye mwamba isiyo na udongo wa kutosha. Zikaota haraka, kwa kuwa udongo ulikuwa haba.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.