Marko 15:39
Mark 15:39 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Basi yule jemadari aliyekuwa amesimama hapo mbele ya msalaba wa Yesu aliposikia ile sauti yake na kuona jinsi alivyokata roho, akasema, “Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu!”
Mark 15:39 in English
Mark 15:39 · Berean Standard Bible
When the centurion standing there in front of Jesus saw how He had breathed His last,* he said, “Truly this man was the Son of God!”
Context
37Kisha Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho. 38Pazia la Hekalu likachanika vipande viwili kuanzia juu hadi chini. 39Basi yule jemadari aliyekuwa amesimama hapo mbele ya msalaba wa Yesu aliposikia ile sauti yake na kuona jinsi alivyokata roho, akasema, “Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu!” 40Walikuwepo pia wanawake waliokuwa wakiangalia kwa mbali. Miongoni mwao walikuwepo Maria Magdalene, na Maria mama yao Yakobo mdogo na Yose, pia na Salome. 41Hawa walifuatana na Yesu na kushughulikia mahitaji yake alipokuwa Galilaya. Pia walikuwepo wanawake wengine wengi waliokuwa wamekuja pamoja naye Yerusalemu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.